Pages

Monday, August 20, 2012

Mgodi wa Marikana waanza kazi tena

UCHAGUZI SOMALIA WAHAIRISHWA

Mwanamke wa Kisomali akiwa na bendera ya nchi yake
Uchaguzi wa rais wa Somalia uliokuwa umepangwa kufanyika Jumatatu hii umeahirishwa. Wabunge wapya wa nchi hiyo wataapishwa na kukutana leo. Tarehe mpya ya uchaguzi haijatolewa.
Wakielezea sababu ya kuahirisha uchaguzi huo, wabunge wa Somalia wamesema kwamba bado kuna maandalizi yanayotakiwa kufanyika kabla ya rais mpya kuchaguliwa. Sultan al-Farahseed ambaye ni msemaji wa rais aliyeko madarakani sasa, Sheikh Sharif Sheikh Hamad, ameeleza kwamba wabunge wa Somalia watakula kiapo leo. Bunge la Somalia litakuwa na wawakilishi 275 pamoja na baraza la senate lenye wanachama 54. Wabunge wote walichaguliwa na viongozi wa jadi na kupitishwa na kamati maalum ya uchaguzi.
"Katika siku chache zijazo, bunge jipya litamchagua spika wake na baada ya hapo, bunge litandaa kamati maalum ya uchaguzi wa rais," alieleza Abinasir Garale, mmoja wa wabunge wapya. Tamko la pamoja lililotolewa na Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na Marekani limeuelezea uchaguzi wa Somalia kama nafasi nzuri ya kuleta usalama. Tamko hilo limesema pia, kwamba kumalizika kwa muda wa serikali ya mpito ni mwanzo wa serikali mpya itakayowawakilisha raia vizuri zaidi. Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanahofia kwamba hakutakuwa na mabadiliko yoyote baada ya bunge kuapishwa na rais mpya kuchaguliwa.
Miongo miwili ya machafuko

Dikteta Mohammed Siad Barre wa Somalia Dikteta Mohammed Siad Barre wa Somalia
Tangu kung'olewa madarakani kwa dikteta Mohamed Siad Barremwaka 1991, Somalia haijawa tena na serikali imara. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vimekuwa vikitawala tangu wakati huo.
Sheikh Ahmed, ambaye amekuwa madarakani kuanzia mwaka 2009, ndiye anayepewa nafasi kubwa zaidi ya kuibuka kidedea katika uchaguzi wa rais, licha ya kwamba Umoja wa Mataifa umeushutumu utawala wake kwa ulaji rushwa. Hata hivyo, kiongozi yeyote atakayekuwa rais, atautawala tu mji mkuu Mogadishu pamoja na maeneo mengine yaliyo karibu. Eneo la kati na la kusini kwa sehemu kubwa liko chini ya utawala wa kundi la kigaidi la al-Shabaab, wakati eneo la kaskazini likiwa chini ya mamlaka ya viongozi wanaotaka kuwa na eneo lao huru.
Wasomali waishio nje ya nchi hawana matumaini

Titel: 1616 Abukar Sheikh Ali vor Skyline 03
Schlagworte: 
Wer hat das Bild gemacht/Fotograf?: Bettina Rühl 
Wann wurde das Bild gemacht?: 30.07.2012
Wo wurde das Bild aufgenommen?: Eastleigh, Stadtviertel von Nairobi/ Kenia 
Bildbeschreibung: Bei welcher Gelegenheit / in welcher Situation wurde das Bild aufgenommen? Wer oder was ist auf dem Bild zu sehen? Der somalische Geschäftsmann und Hotelmanager Abukhar Sheikh Ali über den Dächern von Eastleigh, dem somalischen Viertel in der kenianischen Hauptstadt Nairobi

Abukar Sheikh Ali akiwa jijini Nairobi, Kenya
Kuotokana na mgogoro ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi, raia wengi wa Somalia wameihama nchi yao na kukimbilia nchi jirani. Abukar Sheikh Ali ni mmoja wao. Hivi sasa anaishi nchini Kenya. Familia yake ni ya wafanyabiashara. Wanafanya shughuli zao katika nchi mbali mbali zikiwemo Kenya, Djibouti, Sudan Kusini, Uganda na Dubai. Hata hivyo, Sheikh Ali anaeleza kwamba amepata hasara kubwa Somalia, baada ya hoteli yake iliyokuwa Mogadishu, kubomolewa. Hasara aliyoipata ni takriban dollar za Kimarekani millioni 16.
"Eneo lililo salama zaidi mjini Mogadishu ni lile lililo karibu na uwanja wa ndege," anaeleza Sheikh Ali. Hii ni kwa sababu huko ndiko anakoishi rais pamoja na mawaziri walio wengi. "Maeneo mengine ya Mogadishi, hasa eneo la Magharibi bado ni hatari sana. Bado wapo baadhi ya wafuasi wa kundi la al-Shabaab wanoishi huko." Mfanyabiashara huyu haamini kwamba uchaguzi wa rais mpya utaleta mabadiliko nchini mwake.

Saturday, August 18, 2012

What will you do on August 19th? This World Humanitarian Day I’m doing something good, somewhere, for someone else


This World Humanitarian Day, we want to make a statement that can't be ignored.

We want the world to say 'I WAS HERE', and on August 19th commit to doing something good, somewhere, for someone else.

From major international humanitarian operations to handing out food to the homeless, however big or small let's show the world that we believe in helping others.

But for the world to take notice, we need to shout it loud, all at once.

Join the UN, Beyoncé and global aid organizations in helping to reach 1 billion people, on 1 day, with 1 message by signing up to this Thunderclap.

And on August 19th, we will flood the world with our message.



What will you do on August 19th?


Friday, August 17, 2012

Wachimba migodi 30 wapigwa risasi


Polisi wawafyatulia risasi wachimba mgodi
Zaidi ya watu 30 wauwawa katika makabiliano kati ya polisi na wachimba migodi wanaogoma Afrika kusini.
Waziri wa Polisi wa Afrika kusini amesema maafa hayo yalitokea siku ya Alhamisi katika mgodi wa Marikana.
Polisi walifyatua risasi baada ya kushindwa kuwatawanya wagomaji hao waliokuwa wamejihami kwa marungu na mapanga.
Mgodi huo wa dhahabu nyeupe unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin imekuwa ni sehemu ya mapigano makali kuhusu mzozo wa malipo uliotokana na uhasama kati ya vyama viwili vya wafanyakazi.
Kisa hicho cha polisi ni moja wapo wa operesheni mbaya zaidi ya polisi tangu kumalizika kwa enzi za ubaguzi wa rangi.
Awali machafuko hayo yalioanza wiki iliyopita yalikuwa yamesababisha vifo vya watu 10 na polisi wawili.
Siku ya Ijumaa waziri wa Polisi ,Nathi Mthethwa akizungumza na kituo kimoja cha Radio alithibitisha kuwa watu wengi walijeruhiwa na wengine kuuwawa.
Chama kikuu cha wachimba migodi, National Union of Mineworkers ,kinasema idadi ya waliofariki ni 36.
Polisi walikuwa wamepelekwa kwenda kuwatawanya wachimba migodi wapatao 3,000 ambao walikuwa wamekusanyika eneo la mlima mkabala na mgodi wa Marikana, ambao uko kilomita 100 kaskazini mangharibi mwa Johannesburg.
Wafanyakzi hao walikuwa wanataka nyongeza ya mshahara ya dola $1,000 kila mwezi.
Mazingira yaliofanya polisi waanze kufyatua risasi bado haijajulikana , lakini taarifa kutoka kwa walioshuhudia zinasema mauji hayo yalitokea wakati kundi la waandamani walipojaribu kuwavamia polisi.
Hapo ndipo polisi waliokuwa wamejihami kwa bunduki na bastola wakaanza kufyatua risasi.

Wednesday, August 15, 2012

Muongozo mpya kwa wasafiri wanaotumia meli kwenda Zanzibar


Nchini Tanzania mamlaka inayosimamia misafara ya meli imetoa muongozo mpya kwa ajili ya wasafiri wanaotumia vyombo vya baharini kufuatia mfululizo wa ajali za meli zilizogharimu maisha ya watu.
Je, muongozo huu utapunguza ajali hizi ambazo zinaonekana kukosa ufumbuzi kwa sasa? Iddi Ssessanga amezungumza na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Azam Marine na Coastal Ferries, Hussein Mohammed Said, na kwanza alianza kumuelezea madhumuni ya muongozo huo.


Sikiliza mazungumzo kati ya Iddi Ssessanga na Hussein Mohamed Said

Chanjo ya Ebola huenda isipatikane

  Virusi vya EbolaVirusi vya Ebola

Wanasayansi wanaoendesha utafiti kuhusu virusi vinavyosababisha ugonga wa Ebola, wameiambia BBC kuwa, chanjo inayoweza kutumiwa kuzuia maambukizi ya virusi hivyo huenda isifumbuliwe.
Wiki chahche zilizopita idara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, ilisitisha ufadhili wake kwa kampuni mbili ambazo zilikuwa zikiendesha utafiti huo.
Mmoja wa wataalamu katika jopo hilo amesema kuna uwezekano mkubwa wa chanjo hiyo itakayotumiwa kuzuia mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola haitatumika.
Ugonjwa wa Ebola umetajwa kama moja ya magonjwa hatari na ya kuogofya zaidi ulimwenguni.
Virusi hivyo vinasababisha homa kali ambayo hufanya mtu kuvuja damu katika viungo vya ndani na hata kupitia sehemu zingine kama vile masikio, mapua na hata ngozi.
Wataalamu wanasema virusi hivyo ambavyo hushambulia chembe chembe nyeupe na mishipa ya damu na kusababisha mwasho wa ngozi, macho mekundu, kutapika na mauimivu ya viungo.
Katika miezi ya hivi karibuni watu 16, waliaga dunia Magharibi mwa Uganda, kutokana na ugonjwa huo.
Kufikia sasa hakuna tiba kamili ya ugonjwa huo ambao unaweza kusababisha vifo kwa asilimia 90 ya watu walioambukizwa virusi hivyo.
Mikakati ya kujaribu kufumbua chanjo ya kutibu na kuzuia virusi vya Ebola imefadhiliwa na Idara ya Ulinzi na Taasisi ya Kitaifa ya Afya nchini Marekani NIH.
Idara hizo mbili zimewekeza mamilioni ya dola kwa utafiti huku zikiwa na wasi wasi kuwa virusi hivyo vinaweza kutumiwa kama silaha za kibiolojia.
Kutokana na ufadhili huo, chanjo kadhaa zimefumbuliwa na tayari zimefanyiwa majaribio kwa wanyama na matokeo yake yamekuwa ya kuridhisha.
Kampuni mbili Sarepta na Tekmira tayari zimeanzisha majaribio ya tiba hiyo kwa binadamu.
Lakini kampuni hizo zimefahamaishwa na Idara ya Ulinzi ya Marekani kusitisha utafiti huo mwa muda kutokana na ukosefu wa fedha.
Uamuzi wa mwisho kuhusu ikiwa ufadhili huo utarejelewa tena utatolewa mwezi ujao.

Robin Van Persie waving goodbye to Arsenal

 RVP waving goodbye to Arsenal

RVP atakuwa tegemezi wa tatu kuihama Arsenal ndan ya msimu mmoja

Kwanini unaodoka, bado nakuhitaj? wenger told RVP
Robin Van Persie will be allowed to leave Arsenal and join Manchester United in a £22 million deal.

Monday, August 13, 2012

Kiprotich Arudi nyumbani ( Uganda) na medali ya dhahabu kutoka Landon kwenye mashindano ya Olympic

Stephen Kiprotich (kushoto) akiwe amevaa medali yake ya dhahabu london 2012; John Akii-Bua (kulia) akiwa na medali ya dhahabu  Munich  1972

Kumuona Stephen Kiprotich  ameshinda medal ya dhahabu ni tukio kubwa na la kujivunia kwa wauganda wote, hasa familia ya marehemu John Akii-Bua.

Kiprotich ameizawaida nchi yake medali ya dhahabu baada ya miaka 40, kushirik na kuikosa medali hiyo, Kiprotich amekuwa Mganda a pili kuipatia nchi yake medali ya dhahabu, Mwaka 1972  John Akii-Bua alikuwa Mganda wa kwanza kuipatia nchii hiyo medali kama hiyo kwenye mashindano ya Olympic yaliyofanyika huko Kusini mwa German (Munich), ambapo alishiriki mbio za mita 400 na kushinda.

"Nilisimama karibu na kiti, watoto wangu wakajua mama kakasirika" Denise Akii-Bua Haris, mtoto wa mganda wa kwanza kuipatia nchi yake medali ya dhahabu, akiliambia shirika la habari la BBC akiwa anaangalia ushindi wa Kiprotich.

Nilishangilia sana nilifurahi sana kuona bendera yetu inainuliwa juu, machozi yalinitoka, nilikuwa na furaha sana. Baba angejivunia sana kuwa na Kiprotich.

"Ni muda mrefu sana tumeisubiri siku hii" Medali ya dhahabu ina maana sana kwa nchi yetu, akasema kwanzia sasa wauganda tunaweza kusema tunatokea kule Kiprotich alipotokea.

TUNAJIFUNZA NIN WATANZANIA KUTOKANA NA USHINDI WA STEPHEN KIPROTICH?



Helikopta za kivita za Uganda zapatikana




Msemaji wa Jeshi Uganda ,Kanali Felix Kulaigye
Jeshi la Uganda limesema kuwa helikopta zake nne zilizokuwa zime ripotiwa kutoweka zikiwa njiani kuelekea nchini Somalia sasa zimepatikana na marubani wake wote wako salama.
Akizungumza na BBC msemaji wa jeshi hilo Kanali Felix Kulaigye hakuweza kusema ndege hizo ziko wapi kwa sasa.
Naye msemaji wa jeshi la Kenya, Bogita Ongeri ameiambia BBC kwamba operesheni ya kutafuta ndege hizo ilikuwa imevurugwa na hali mbaya ya hewa na kuongeza kuwa helikopta hizo nne zilikuwa kwenye safari hiyo kutoka nchini Uganda.
Moja ya helikopta hizo ilitua katika mji wa Garissa.
Rubani aliyekuwa kwenye helikopta ya pili alizungumza na mamlaka za kenya akisema yuko katika eneo la mlima kenya lakini hakukukuwa na mawasiliano na helikopta nyingine mbili.
Helikopta hizo za Uganda hutumiwa kusindikiza misafara kutoka angani, katika opereresheni za utafutaji na uokoaji pamoja na kushambulia wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabaab nchini Somalia.
Helikpta hizo ni miongoni mwa ndege ambazo zilikuwa zikielekea Somalia kukipa nguvu kikosi cha Umoja wa Afrika .
Awali msemaji wa jeshi la Uganda Kanali Felix Kulayigye alikuwa amesema kuwa walikuwa wakizitafuta ndege zao mbili aina ya Mi-24 . Alisema ndege hizo ni zile za kufanya mashambulizi.