Kampuni kubwa ya uchimbaji wa madini ya Platinum, Lonmin,
imeufungua tena mgodi wake wa Marikana, nchini Afrika ya Kusini.
Kumefunguliwa kwa mgodi huo kumekuja takribani wiki moja, baada
ya wafanyakazi 34 kupigwa risasi na kuuawa na polisi, wakati
wakiwa kwenye mgomo. Karibu robo tatu ya wafanyakazi wamerudi
kazini na shughuli za uchimbaji zimeanza tena. Kampuni hiyo
imewapa wafanyakazi waliosalia hadi leo kuwa wamesharudi kazini,
vyenginevyo wafukuzwe kazi. Muda huo ulikuwa umewekwa kuwa
jana, lakini mmiliki wa Lonmin akauongeza kwa masaa 24 zaidi.
Wiki iliyopita ilishuhudia machafuko makubwa kabisa kati ya polisi na
kiasi ya wachimba madini 3,000 kwenye mgodi huo. Polisi inasema
ilikuwa ikijilinda dhidi ya wafanyakazi waliokuwa na mapanga na
bastola. Watu wengine 10 walikufa mwanzoni mwa maandamano
hayo yaliyochochewa na mzozo wa malipo. Rais Jacob Zuma
ameagiza kufanyika kwa uchunguzi na kutangaza wiki moja ya
maombolezo ya kitaifa.
No comments:
Post a Comment