§Kama mwanadamu wa kawaida inakupasa uwe unazingatia nguzo nne za uwanadamu.
§Nguzo ambazo zitakufanya uishi milele kwa amani na furaha, kwa uwapendao na matumaini, bila buguza wala malalamiko, ukiwa na furaha moyoni na rohoni.
•Nguzo hizo ni mara chache na wanadamu wachache wameweza kuzizingatia na wamefanikiwa kwa kila nyanja za kimaendeleo.
•Nguzo nne ambazo zimekuwa ni ngumu kwa mwanadamu kuzizingatia na kuzifuatila.
Nguzo hizo ni
1.ELIMU
2.DINI
3.KUTUNZA MWILI NA
4. JAMII.
•Hayo yote ni mambo ya kawaida kwa mwanadamu yeyote na si mara ya kwanza kupata yasikia ama kuelezewa, lakini mambo ya muhimu na ya kuzingatiwa ili utimize uwanadamu wako.
1. ELIMU
•Elimu ni muongozo muhimu wa mwanadamu, kwani unatupatia
ufumbuzi wa mambo mbalimbali, ujuzi, na kutufanya tuishi kwa amani, upendo na furaha miongoni mwetu.
•Elimu imegawanya katika makundi mawili yaani, elimu ya dini na elimuya kidunia.
•Kama ukiniambia niseme ipi ni bora ningeshindwa kuchangua maana zote zinategemeana na zina umuhimu kwetu.
a. ELIMU YA DINI
•Elimu ya dini ni yale mafundisho tunayopatiwa na Mwenyezi MUNGU kupitia vitabu vitakatifu vilivyo andikwa na manaabii na mitume wetu waliopata ishi ulimwenguu, mafundisho hayo tunapatiwa, kukumbushwa na kuelimishana na viongozi wetu wa dini.
•Elimu hii hutuwezesha na kutenda mambo mazuri na yanayopaswa kutendwa na mwanadamu, mfano:- kuweza msamehe mwenzako endapo atakukosea, kuweza mpenda mwenzako kama unavyojipenda wewe, na upendo ndiyo kitu kikubwa ambacho kinabeba ujumbe katika Elimu ya dini.
b. ELIMU YA DUNIA
Elimu ya kidunia ni ule ujumbe, ujuzi ama mafundisho tunayoweza pewa na wakufunzi wetu ilituweze kabiliana na mazingira kwa ujumla.
Elimu ya Kidunia inawiana
na elimu ya kidini, na kwa uwalisia sehemu kubwa ya elimu ya kidunia imetokana na elimu ya dini.
Kwahiyo unakuja kukuta kuwa zote kwa pamoja zinategemeana katika kumsaidia mwanadamu kuweza kukabiliana na hali alisi ya mazingira anayoishi.
UMUHIMU WA ELIMU
•Mwanadamu yakupasa itafute elimu na kuitumia katika mambo yako mbalimbali ya kila siku, kwani dhumuni la kupatiwa elimu ni kuweza kukabiliana na mazingira yanayotuzunguka.
•Vitabu vyetu vitakatifu vinatuonesha na kutuelewesha matakwa ya Mungu kwa mwanadamu ni pamoja na kiitafuta na kiitumia elimu. “ Bila kuwa na elimu tutashindwa Ishi”
2. DINI
•Dini ni njia inayomuongoza mwanadamu kuweza kuwasiliana na Mwenyezi Mungu, kwa njia mbali mbali, ikiwamo njia ya sala na maombi.
•Kihistoria dini ndiyo, wanadamu walikuwa wakiwasiliana na Mwenyezi Mungu, kwa njia ya sauti ijayo masikioni mwako bila jua wapi ilipotoka. Ila mara baada ya wanadamu kumuhudhi na kumkasirisha mwenyezi Mungu, sasa ni wachache wawezao kuwasiliana na mwenyezi Mungu kwa kusikia sauti, ila wengiwetu tunawasiliana kwa njia ya sala (Dua) na maombi.
MATABAKA YA DINI
•Matabaka ya kidini yametokana na imani za wanadamu, kuamini kuwa njia iliyo sahii ni ipi ya yeye kuweza mfikishia salamu zake Mwenyezi Mungu.
•Dini imegawanyika katika makundi matatu nayo ni:-
•DINI YA KIISLAMU
•DINI YA KIKRISTO
•NA WAPANAGI.
UMUHIMU WA DINI
•Umuhimu mkubwa wa kuzingatia dini pamoja na mwanadamu kuweza ishi milele, na kuepuka Adhabu ya milele endapo atatoweka katika ulimwengu huu
(atafariki).
•Inaaminika kuwa endapo utatenda maovu duniani basi huko uendapo utapata mateso ya milele. Ilikuepuka hayo inakupasa uishike na kuitumia dini, kuishika na muitumia huku kwa dini ni pamoja na kuzizingatia na kuzitumia amri kumi za Mwenjezi Mungu kama muongozo wako wa kimaisha.
3. JAMII
•Kuishi vizuri na watu wanaokuzunguka ni jambo la muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Kuishii vizuri ni pamoja na kuweza msaidia mwanadamu kuweza wasiliana na kusaidiana, kufarijiana
na kufurahia mambo mbalimbali ya kiamaendeleo.
•Mafanikio ya mwanadamu hutegemea uwepo wa Mungu na jitihada za mwanadamu katika kujituma kufikia malengo yale aliyojiwekea, ila mwanadamu pia anategemea mwanadamu mwenzake ilikufanikiwa na kufikisha malengo hayo.
•Hivyo mwanadamu inampasa kuishi vizuri na mwenzake.
•Kwani mwanadamu peke yako ni vigumu kuweza fanya vitu vyote peke yako, bali unahitaji msaada ili uweze fanya mambo mbalimbli.
•Ndio maana kwenye jamii zetu kuna baba, mama. Watu wanaweza funga pingu za maisha wakiapa kusaidiana na kupendana milele.
•“kama mwanadamu yakupasa uweze ishi vizuri na jamii inayokuzunguka”
4. MATU,IZI MAZURI YA MIILI YETU
•Ilikuweza
kutimiza wajibu wetu hapa Duniani yatupasa kuweza tunza miili yetu, kuweza epukana na magonjwa.
•Njia mojawapo ya kuepukana na magonjwa na kutunza miili yetu ni pamoja na kuweza fanya mazoezi ya mwili mara ka mara maana hii hutuwezesha kuepukana na magonjwa ya kunyemelewa kama, homa, kisukari, ugunjwa wa moyo na saratani.
Mazoezi huweza tusaidia kuweza kukuza miili yetu, kuikomaza na kukufanya uwe mwepesi.
Mazoezi huweza tusaidia kuweza kukuza miili yetu, kuikomaza na kukufanya uwe mwepesi.
HITIMISHO
•Nivigumu kuweza chagua, ipi ni nguzo muhimu na inayofaa kuifuata, na ipi kuiacha, ilikuweza ishi maisha mazuri milele.
•“ Ukweli ni kwamba nguzo zote nne zinategemeana na zinauzito sawa”
•Haikupaswi kama mwanadamu kuacha/ kuepuka nguzo hata moja, maana zote nne zinategemeana.
•Mfano: moja wetu aamuwe kufuata elimu pamoja na dini, huyu ataitajika katika sehemu hizo mbili na hatakuwa na afya nzuri, hivyo hataishi maisha marefu, kwani ataandamwa na magonjwa na hatakuwa na mahusiano mazuri na wanadamu wenzake.
•Mfano 2:
•Na mwingine akaamua kutunza mwili wake, huyu atateketeza robo tatu ya umuhimu wake hapa duniani, maana huyu ataitajika sehemu za ulinzi zaidi, na ikifika wakati ametumiwa barua atashindwa soma, hivyo ataitaji, mwenye elimu ya kusoma na muandika aje amsomee na amuandikie.
•Na hataweza fika sehemu pazuri endapo amefariki kwani alishindwa ishika na kiifuata dini.
TAFAKARI CHUKUA HATUA
•Kutokana na hayo unakuja jua nguzo zote nne ni muhimu na za msingi kama mwanadamu kuweza zifuata.
•“ndugu zangu mwenye macho aambiwi tazama na mwenye masikio aambiwe sikia”
No comments:
Post a Comment