Pages

Wednesday, November 30, 2011

TUIJENGE TANZANIA

TOFAUTI KATI YA NCHI TAJIRI NA MASIKINI SIO KUWA NA UHURU KWA MUDA MREFU.

  • Kwa mfano Ethiopia na Liberia, ambazo hazikutawaliwa barani Africa lakini bado hazijaendelea(maskini).
  • K wa upande mwingine nchi kama Corea, South Africa, Canada na Austaria ambazo zilipata uhuru miaka 150 iliyopita lakini ni nchi zilizoendelea (mf. South ilipata uhuru 1990).

TOFAUTI KATI YA NCHI MASIKINI NA TAJIRI HAIPO KWENYE UPATIKANAJI NA UWEPO WA MALIASIRI.

  • Kwa mfano, Japan ambayo 80% ya eneo lake ni milima na haina eneo la kulima au kufugia mifugo, lakini ni nchi ya tatu duniani kwa utajiri, inaingiza maligafi (raw material) kutoka pande zote za dunia na inazalisha bidhaa( manufactured products) kwenda pande zote za dunia.
  •    mf. mwingine ni Swit zerland, ambayo hailimi cocoa lakini inazalisha chocolate bora duniani. katika eneo lake dogo inafuga mifugo na inalima misimu minne(4) kwa mwaka.

UTOFAUTI UNAKUJA WAPI SASA?

Utofauti ni ile tabia ya watu, walivyojijengea  akilini mwao kutokana na elimu wanayopata na utamaduni wao.

Katika kuzichambua tabia za watu wanaoishi nchi zilizoendelea na tajiri, unafahamu kuwa wao walizingatia haya yafuatayo:-
  1. kujifunza  kuwa kipini kizuri na kipi ni kibaya katika jamii ya mwanadamu. (ethics) hii ilkuwa sheria kubwa walioitumia.
  2. kuwa na matamanio ya mambo makubwa (will of super action).
  3. punctuality.
  4. KUHESHIMU NA KUZIFUATA SHERIA NA KANUNI WALIZO JIWEKEA.
  5. KUFANYA KAZI KWA UPENDO.
  6. KUTEKELEZA MAJUKUMU KWA KILA MMOJA KULINGANANA WADHIFA WAKE.
  7. na KUHESHIMU HAKI ZA KILA MWANANCHI.
Katika nchi masikini ni wachache wanatekeleza hayo katika taratibu zao za kila siku.

WATANZANIA SIO MASIKINI KWA SABABU HATUNA MALIGHAFI.
Watanzania ni masikini kwa sababu hatuna matarajio ya kufanya kitu kikubwa, hatutekelezi majukumu yetu ipasavyo.
KWA UZALENDO WA KUIPENDA NCHI YAKO, WATUMIA MARAFIKI UJUMBE HUU, NAWE PIA UUFUATE ILI TUIBADILISHE TANZANIA.
                                              MUNGU IBARIKI AFRICA
                                MUNGU IBARIKI TANZANIA.

No comments: