Pages

Monday, August 13, 2012

Kiprotich Arudi nyumbani ( Uganda) na medali ya dhahabu kutoka Landon kwenye mashindano ya Olympic

Stephen Kiprotich (kushoto) akiwe amevaa medali yake ya dhahabu london 2012; John Akii-Bua (kulia) akiwa na medali ya dhahabu  Munich  1972

Kumuona Stephen Kiprotich  ameshinda medal ya dhahabu ni tukio kubwa na la kujivunia kwa wauganda wote, hasa familia ya marehemu John Akii-Bua.

Kiprotich ameizawaida nchi yake medali ya dhahabu baada ya miaka 40, kushirik na kuikosa medali hiyo, Kiprotich amekuwa Mganda a pili kuipatia nchi yake medali ya dhahabu, Mwaka 1972  John Akii-Bua alikuwa Mganda wa kwanza kuipatia nchii hiyo medali kama hiyo kwenye mashindano ya Olympic yaliyofanyika huko Kusini mwa German (Munich), ambapo alishiriki mbio za mita 400 na kushinda.

"Nilisimama karibu na kiti, watoto wangu wakajua mama kakasirika" Denise Akii-Bua Haris, mtoto wa mganda wa kwanza kuipatia nchi yake medali ya dhahabu, akiliambia shirika la habari la BBC akiwa anaangalia ushindi wa Kiprotich.

Nilishangilia sana nilifurahi sana kuona bendera yetu inainuliwa juu, machozi yalinitoka, nilikuwa na furaha sana. Baba angejivunia sana kuwa na Kiprotich.

"Ni muda mrefu sana tumeisubiri siku hii" Medali ya dhahabu ina maana sana kwa nchi yetu, akasema kwanzia sasa wauganda tunaweza kusema tunatokea kule Kiprotich alipotokea.

TUNAJIFUNZA NIN WATANZANIA KUTOKANA NA USHINDI WA STEPHEN KIPROTICH?



No comments: